Mwigizaji huyu
maarufu wa filamu kutoka Marekani, Denzel Washington ameweka wazi kuwa
kwa sasa anapambana sana ili kujizuia kunenepa kupita kiasi hasa
kutokana na tabia yake ya kupenda kula sana vitu vyenye sukari hususan
Ice Cream mbaya zaidi ikiwa ni katika wakati huu ambao muda mrefu anakua
amejifungia ndani ku-edit filamu.
Msanii
huyu amesema katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni kuwa kuna
kipindi hali ilikuwa mbaya hasa baada ya kuongezeka sana wakati
alipokuwa na kazi ya kuongoza filamu na baadaye kukaa katika kipindi cha
miezi sita kui-edit na kuiweka sawa ambapo aliponzwa sana na tabia yake
ya kupenda kula.
Kwa sasa msanii huyu
yupo katika ratiba kali ya mazoezi ili kudhibiti hali hii inayomtesa na
pia akiwa katika maandalizi ya kukamilisha filamu yake mpya ambayo
itakwenda kwa jina 2 Guns ambayo inasubiriwa kwa hamu.
Aucun commentaire